Ruto apiga kura Rift Valley

0
189

Mgombea wa kiti cha Urais nchini Kenya kutoka Muungano wa Kenya Kwanza – Naibu Rais wa nchi hiyo William Ruto amesema, ana matumaini makubwa ya kushinda kiti hicho.

Ruto ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kupiga kura katika mkoa wa Bonde la Ufa, ambako ni nyumbani kwake.

Amesema leo ni siku kubwa kwake sababu anaamini atashinda, na ana imani kubwa Wakenya watampa nafasi ili aweze kuwatumikia.

Hii ni mara ya kwanza kwa William Ruto mwenye umri wa miaka 55 kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha Urais baada ya kuwa Naibu Rais wa Kenya kwa muda wa miaka 10.

Kiti cha urais nchini Kenya kinawaniwa na wagombea wanne, lakini upinzani mkubwa ni kati ya Ruto na Raia Odinga kutoka Muungano wa Azimio la Umoja ambaye anashiriki katika kinyang’anyiro hicho kwa mara ya tano.