Russia, Uturuki na Iran kumaliza mapigano Syria

0
1089

Rais Vladimir Putin wa Russia  amewahimiza viongozi wenzake wa Uturuki na Iran kushirikiana ili kumaliza mapigano yanayoendelea nchini Syria.

Rais Putin ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na  Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Hassan Rouhani wa Iran katika mji wa Sochi.

Putin amewaambia viongozi hao kwamba jambo la haraka wanalotakiwa kushirikiana  ni kupambana na vikosi vya Waasi vilivyopo katika jimbo la Idlib ambavyo vimekua vikiendeleza mapigano.

Syria  imekua katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka saba na kusabababisha mauaji ya maelfu ya watu.