Rapa wa Marekani William Leonard Roberts II maarufu kama Rick Ross, anatarajia kupanda mlima Kilimanjaro mwaka 2024.
Katika mahojiano kwenye kipindi cha mtandaoni cha ‘Full Send Podcast’, rapa huyo amewaeleza watangazaji wa kipindi hicho Kyle Forgeard na Bob Menery kwamba matamanio yake ni kupanda mlima huo ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika.
“In 2024 I’mma hike to the top of Kilimanjaro.” akimaanisha ” mwaka 2024 nitapanda hadi kilele cha mlima Kilimanjaro.
Rick Ross amewahamasisha mastaa wengine duniani kuungana naye katika tukio hilo.
Mastaa wengine waliowahi kupanda mlima Kilimanjaro ni pamoja na Roman Abramovich ambaye ni mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya Chelsea, muigizaji wa filamu wa nchini Marekani, Jessica Timberlake, rapa Lupe Fiasco pamoja na muigizaji Mandy Moore.