Rais wa Sierra Leone kufunga ndoa mara ya pili

0
553

Sauti za kengele za harusi zitalia leo katika Mji Mkuu wa Sierra Leone, Freetown, wakati Rais wa nchi hiyo, Julius Bio atakapokuwa akifunga ndoa na mke wake.

Rais Bio na mkewe Fatima Bio watabadilisha viapo katika Kanisa Katoliki, wakati watakapokuwa wakifunga ndoa ya kikanisa, ikiwa ni miaka saba baada ya kufunga ndoa ya kiserikali nchini Uingereza.

Mke wa kwanza wa kiongozi huyo amedai kuwa alifunga naye ndoa ya kidini, lakini msajili wa ndoa katika kanisa hilo amesema kuwa hakuna rekodi ya ndoa hiyo.

Ndoa ya Rais Bio imeibua mjadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wananchi wanatoa maoni yao, huku wengi wakiisubiria kwa hamu.