Rais wa Hungary ziarani Tanzania

0
273

Rais Katalin Novak wa Hungary anatarajiwa kuwasili nchini leo jioni kwa ziara ya kikazi ya siku nne kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Atakuwa nchini kuanzia leo Julai 17 hadi Julai 20, 2023.

Katalin Novak ni mwanasiasa maarufu nchini Hungary ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa Taifa hilo katika uchaguzi wa mwaka 2022.

Ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Urais nchini Hungary na pia ndiye Rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Alichaguliwa akiwa na umri wa miaka 44 na kabla ya kushika wadhifa huo, alikuwa Waziri anayehusika na Sera za Familia.