Rais Trump aanza ziara Uingereza

0
535

Rais Donald Trump  wa Marekani na Mke wake Melania Trump wapo nchini Uingereza, ambapo Trump ameanza ziara ya siku Tatu nchini humo.

Wakati wa ziara yake nchini Uingereza, Trump  anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo anayeondoka madarakani Theresa May na viongozi wengine.

Habari zaidi kutoka nchini Uingereza zinasema kuwa,  Raia kadhaa wa nchi hiyo wamepanga kuandamana katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na London, Manchester, Belfast na Birmingham kupinga ziara hiyo ya Rais Trump.