Rais Samia : Uchaguzi umekwisha mkajenge Taifa

0
626

Rais Samia Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa raia wote wa Kenya kushikamana na kulijenga Taifa lao.

Rais Samia ametoa kauli hiyo katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi nchini Kenya, wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua.

Amesema uchaguzi umekwisha, na kikubwa kwa raia wote wa Kenya ni kushikana mikono na kusonga mbele.

Ameihakikishia Kenya ushirikiano, ili kuleta maendeleo ya pamoja kati ya pande hizo mbili na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kwa mara nyingine tena, Rais Samia amempongeza Rais William Ruto na Naibu wake kwa kuchaguliwa kuliongoza Taifa hilo, na pia amempongeza Rais aliyeondoka madarakani Uhuru Kenyatta kwa kuongoza Taifa hilo kwa amani na utulivu.