Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Namibia (Diaspora).
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Windhoek.
Dkt. Samia amezungumza na Watanzania hao wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika na nchi zinazochangia vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB).