Rais Samia Suluhu Hassan leo amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza aliyefariki dunia tarehe 8 mwezi huu.
Rais Samia amesaini kitabu hicho katika jengo la Lancaster London, Uingereza.
Rais Samia Suluhu Hassan pia ameungana na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Malikia Elizabeth II kabla ya kufanyika kwa mazishi ya kitaifa huko Westminster Abbey hapo kesho.