Rais Museveni aapishwa

0
335

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameapishwa kushika rasmi wadhifa huo kwa muhula wa sita.

Rais Museveni ameapishwa kushika wadhifa huo kufuatia ushindi wa asilimia 58.64 ya kura zote alizopata kwenye uchaguzi uliofanyika nchini Uganda Januari 14 mwaka huu, na kushirikisha zaidi ya wagombea kumi wa Urais.

Sherehe za kumuapisha Rais Museveni zimefanyika katika uwanja wa Kololo uliopo Kampala na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

Rais Yoweri Museveni aliyezaliwa mwaka 1944, ameliongoza Taifa la Uganda kwa takribani miaka 35.

Alichukua madaraka mwaka 1986 baada ya kushinda vita vya msituni chini ya kundi la National Resistance Movement (NRM).