Rais Mteule wa Chad afariki dunia

0
148

Rais Mteule wa Chad Idriss Deby amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapambano dhidi ya Waasi.

Rais Deby amefariki dunia saa chache baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuwa mshindi wa kiti cha Urais kufuatia uchaguzi uliofanyika tarehe 11 mwezi huu.