RAIS GEINGOB AUNGA MKONO SERA NA MSIMAMO WA RAIS MAGUFULI

0
308

Rais wa NAMIBIA na Mwenyekiti wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika – SADC anayemaliza muda wake Dkt. HAGE GEINGOB, amesema anaunga mkono msimamo wa Rais Dkt. JOHN MAGUFULI katika falsafa ya kuimarisha viwanda kwa nchi za SADC ili kuchochea maendeleo ya haraka na kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa wananchi.

Rais GEINGOB amesema hayo leo katika mahojiano maalum na Mwandishi wetu Gabriel Zakaria katika Ikulu ya mjini WINDHOEK NAMIBIA na kumtakia kila la kheri Mwenyekiti mpya ajaye Rais DKT. JOHN MAGUFULI.

Aidha Akikabidhiwa zawadi na mmoja wa Wafanyakazi wa TBC kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu DKT. AYUB RIOBA, Rais Dkt. GEINGOB ameushukuru uongozi wa TBC kwa kumpa zawadi na kuahidi kutumia moja ya kikombe alichopewa kila siku anapopata kifungua kinywa.