Rais Buhari aapishwa

0
477

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameapishwa kuliongoza Taifa la Nigeria kwa kipindi cha Pili, katika sherehe zilizofayika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Abuja.

Wakati wa kula kiapo hicho, Rais Buhari mwenye umri wa miaka 76  alivalia vazi la kiasili la nchi hiyo huku sherehe hizo zikihudhudhuriwa na idadi kubwa ya Raia wa Nigeria.

Yemi Osinbajo, naye ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Nigeria kwa kipindi cha Pili.

Rais Buhari ameapishwa baada ya kupata ushindi wa kiti cha Urais,  kufuatia uchaguzi uliofanyika mwezi Februari mwaka huu  ambapo alipata asilimia 56 ya kura zote zilizopigwa dhidi ya asilimia 41 ya kura alizopata mpinzani wake wa karibu Atiku Abubakar.

Wakati wa kampeni za uchaguzi, Buhari alikua akishutumiwa kwa kushindwa kushughulikia uchumi wa nchi hiyo unaoonekana kuyumba, kushindwa kushughulikia vitendo vya rushwa na kushindwa kuimarisha hali ya usalama wa nchi hiyo.