Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia amemfukuza kazi Waziri wake Mkuu Mohammed Hussein Roble, kutokana na tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo rushwa na kujitwalia ardhi ya jeshi kinyume cha sheria.
Akitangaza uamuzi huo Rais Abdullahi amesema ameamuru uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma za Roble ambaye ni Kamanda wa zamani wa jeshi la maji la Somalia.
Siku chache zilizopita, Roble ambaye wako katika mzozo wa kugombea madaraka na Rais wake alitangaza vikosi vyote vya jeshi vipokee amri na maelekezo kutoka kwake.
Waziri Mkuu huyo aliyefukuzwa kazi amesema hatua hiyo ni kinyume na katiba ya nchi.
Mzozo kati ya Viongozi hao unatishia amani na utulivu, ikiwemo kuzuka kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia.