Rais achangia milioni 70 kusaidia watoto Njiti

0
63

Rais Samia Suluhu Hassan amechangia shilingi milioni 70 kwenye taasisi ya Doris Mollel Foundation, ambapo shilingi milioni 20 ni kwa ajili ya kuwasaidia watoto Njiti kupitia taasisi hiyo.

Pia Rais Samia amenunua vifa tiba vya kuwasaidia watoto Njiti vyenye thamani ya shilingi milioni 50.

Mkurugenzi wa taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel amemshukuru Rais Samia kwa msaada huo na kuongeza kuwa msaada huo umetolewa katika wakati mwafaka.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, fedha hizo ni za Rais mwenyewe kutoka kwenye mshahara wake na amemshukuru kwa msaada huo.

Ameongeza kuwa serikali kupitia wizara ya Afya itaendelea kuwasaidia watoto Njiti pamoja na wanawake wanaojifungua watoto Njiti.

Taasisi ya Doris Mollel Foundation hapo jana iliadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, maadhimisho yaliyofanyika wilayani Serengeti, mkoani Mara.

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani yalifanyika duniani kote tarehe 17 mwezi huu.