Raila na Ruto wakabana kura za Urais

0
404

Matokeo ya awali yanaendelea kutolewa nchini Kenya, kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika hapo jana.

Katika kinyang’anyiro cha Urais, wagombea wawili ambao ni William Ruto kutoka muungano wa Kenya Kwanza na Raila Odinga kutoka muungano wa Azimio la Umoja wameonekana kuchuana vikali.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, hadi kufikia saa 2:30 asubuhi hii, William Ruto anaongoza kwa kura 683, 779 ambazo ni sawa na asilimia 50 .78 ya kura zote zilizohesabiwa.

Bofya hapa kufuatilia mbashara matokeo ya Uchaguzi Mkuu Kenya

Raila Odinga yeye ana kura 654, 168 sawa na asillmia
48.58 ya kura hizo.

Hata hivyo licha ya matokeo hayo ya awali kuwekwa kwenye mitandao ya Tume hiyo ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, bado tume hiyo haijajitokeza kuyatangaza rasmi.