Raia wa Sudan washinikiza haki kwa waliouawa kwenye maandamano

0
669
REFILE - REMOVING ERRONEOUS WORD Sudanese protesters march during a demonstration to commemorate 40 days since the sit-in massacre in Khartoum North, Sudan July 13, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Baadhi ya raia wa Sudan wameendelea kuishutumu serikali ya nchi hiyo kuwa haijawatendea haki kuhusiana na vifo vya ndugu zao waliouawa wakati wa maandamano yaliyoshinikiza mabadiliko ya kiserikali nchini humo.

Watu hao wamasema kuwa leo wanaadhimisha mwaka mmoja tangu, aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Omar al-Bashir kuondolewa na madarakani lakini bado haki haijatendeka kwa ndugu zao waliofariki wakati wa maandamano yaliyopelekea mapunduzi.

Jeshi la Sudan lilishika hatamu za uongozi baada ya Bashir kuondolewa madarakani, lakini watu wengi waliuawa na jeshi na wengi kutoswa katika Mto Nile, ili kudhibiti maandamano yao ya kupinga utawala wa kijeshi.