Raia mmoja wa Kenya amekamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bangkok uliopo nchini Thailand, -akijaribi kuingiza nchini humo kete 68 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Maafisa wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Thailand waliopo kwenye uwanja huo wamesema kuwa, -Glenn Chibasellow Ookow mwenye umri wa miaka 43 alimeza dawa hizo zenye uzito wa Kilo 1.2.
Raia mwingine wa Nigeria amekamatwa akiwa na dawa za kulevya katika uwanja huo wa Ndege wa Kimataifa wa Bangkok akitokea nchini Kenya, na alikua akiingiza dawa hizo nchini Thailand na katika nchi nyingine jirani na nchi hiyo.
Maafisa wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Thailand waliopo kwenye uwanja huo wameongeza kuwa, kukamatwa kwa watu hao kunaashiria uwepo wa mtandao wa kuingiza nchini humo dawa za kulevya.
Tangu mwezi Oktoba mwaka 2018 hadi hivi sasa, Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Thailand imekamata watu 43 kwa tuhuma za kuingiza nchini humo dawa za kulevya, watu ambao wamekamatwa kufuaia operesheni maalum ya kuwasaka watu wote ambao wamekua wakiingiza nchini humo dawa za kulevya.