Polisi kudhibiti mashambulio London

0
428

Uingereza imeongeza doria ya polisi katika mji wa London ili kukabiliana na mashambulio ya watu wanaotumia visu dhidi ya watu wengine na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia.

Kumekuwa na matukio mengi ya watu kushambuliwa na visu na kuuawa na watu wanaokuwa wamedhamiria kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mji wa London.

Shambulio moja lilitokea baada ya mtu mwenye kisu kuwashambulia watu waliokuwa katika eneo la wazi,  wakisherehekea tamasha la muziki.

Waziri Mkuu wa Uingereza, -Thereza May amelaani mashambulio hayo na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa.

Watu wengi wanaojihusisha na mashambulio hayo ni vijana ambao baadhi yao wanatuhumiwa kutumia dawa za kulevya ambazo zimeathiri ufahamu wao.