Polisi Dubai wamnasa Hushpuppi kwa wizi wa mabilioni

0
897

Polisi mjini Dubai wameachia video inayoonesha jinsi walivyomkata milionea kutoka nchini Nigeria, Hushpuppi anayetuhumwa kwa makosa mbalimbali yekiwemo ya ya wizi mitandaoni na utakatishaji fedha

Mbali na Hushpuppi ambaye jina lake halisi ni Ramoni Igbalode, polisi wanawashikilia watu wengine 11 ambao ni sehemu ya genge la raia huyo wa Nigeria ambaye amejizolea umaarufu mitandaoni kwa maisha yake ya anasa.

Brigedi Jamal Salem Al Jallaf, Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka kitengo cha polisi, Dubai, amesema walipokea habari juu ya genge la watu waliohusika katika utapeli wa pesa mitandaoni.

“Genge hilo ikiwa ni pamoja na Hushpuppi, wanajulikana kwa kuonesha utajiri wao kwenye mitandao ya kijamii na kujinasibu kuwa ni wafanyabiashara ili kuwanasa watu kutoka pande zote za ulimwengu. Timu ya Polisi Dubai ilifuatilia genge hilo ambalo lilikuwa linaunda akaunti kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia majina bandia,” amesema Jallaf amesema.

Hushpuppi mara nyingi huweka picha kwenye ukurasa wake akiwa na gari yake ya kifahari kama Ferrari na Rolls Royce na ndege ya kibinafsi lakini pia huonekana akiwa amevaa nguo za bei ghali za chapa kubwa duniani kama vile Gucci, Versace, Prada, Louis Vuitton na Ralph Lauren.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Hushpuppi amewaibia watu mbalimbali zaidi ya dola za Kimarekani millioni 421 (zaidi ya shilingi Trilioni 1 za kitanzania), kupitia mitandao ikiwemo kughushi tovuti za benki na makampuni mbalimbali pia kucheza na taarifa binafsi za watu mtandaoni na kubadilisha mwelekeo wao wa kutuma pesa na kuzichukua wao.

Katika operesheni iliyopewa jina Hunt Fox 2, polisi wamekamata magari 13 ya kifahari na fedha, Polisi walisema shambulio hilo lilisababisha kukamatwa kwa hati za kuwatia hatiani kuhusu ujangili wa kimataifa uliopangwa vizuri, wenye thamani ya shilingi trilioni 1.1.

Luteni Jenerali Abdullah Khalifa Al Merri, Kamanda-Mkuu wa Polisi wa Dubai, amesema kufanikiwa kwa operesheni hiyo ni nyota nyingi kwenye kofia ya Polisi Dubai.

“Polisi wa Dubai wanasimama kidete dhidi ya utapeli wa pesa na udanganyifu wa mitandao tunatumia teknolojia na mbinu za mpya na kisasa ambazo magenge hutumia katika uhalifu wao. Tuna timu ya maafisa waliohitimu kusimama kidete dhidi ya ujangili,” amesema Merri.