Picha mpya ya Malkia yatolewa

0
164

Kasri la Buckingham limetoa picha mpya ya mwisho ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Picha hiyo iliyopigwa na Ranald Mackechnie, inamuonesha Malkia Elizabeth II akiwa amevalia suti ya bluu bahari huku akitabasamu.

Picha ya Malkia Ilichukuliwa mwaka huu siku ya kuadhimisha Jubilee yake ya Platinum, kwani alikuwa mtawala wa kwanza wa Uingereza kufikia hatua hii muhimu.

Kwenye picha hiyo pia Malkia anaonekana amevalia mkufu wake maarufu sana na vidani vya kubana kwenye nguo ambavyo ni zawadi kutoka kwa baba yake, Mfalme George katika siku yake ya kuzaliwa ambapo kwa wakati huo alikuwa akitimiza umri wa miaka 18.