Serikali ya Philippines imemuita nyumbani Balozi wake aliyeko nchini Canada, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi baada ya Canada kushindwa kuondoa taka kutoka nchini humo ilizozitelekeza.
Philippines iliipatia Canada muda ili kuondoa makontena yake yenye taka yaliyosafirishwa kutoka nchini humo na kwenda kutekelezwa katika pwani ya Philipinnes yakiwa yamepakiwa ndani ya meli mbili, lakini nchi hiyo imeshindwa kuyaondoa.
Makonteina hayo yenye taka ambazo zinasemekana ni hatari, yaligunduliwa nchini Philippines mwaka 2014 wakati wa utawala wa Rais Bennino Aquino.