OMBAOMBA BILIONEA

0
278

Imezoeleka kuwa ombaomba unaokutana nao kwenye maeneo mbalimbali mjini ni watu wa hali duni na hawajikumu kimaisha. Mwonekano wao pia hushabihiana na dhana hiyo.

Ombaomba mmoja mjini Mumbai, India amejikwamua kutoka kwenye dhana hiyo na kujipatia hadhi ya ombaomba tajiri zaidi duniani.

Bharat Jain amejipatia dola milioni 1.3 milioni sawa na shilingi bilioni 3.17 za Kitanzania kwa kuomba katika mitaa iliyoendelea na mji mkuu wa kifedha wa nchi hiyo.

Ni sawa na kusema Jain anapata shilingi 107,360 kwa siku na 3,220,800 kwa mwezi.

Anamiliki ghorofa ya kifahari yenye vyumba viwili, ana maduka mawili na anasomesha watoto shule nzuri lakini amegoma kuacha kuwa ombaomba hata pale alipotakwa kuacha na nduguze.