Odinga: Ni uchaguzi mzuri

0
239

Wananchi wa Kenya wanaendelea kupiga kura katika uchaguzi mkuu nchini humo, ambapo mgombea wa kiti cha Urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga amepiga kura katika kituo kilichopo eneo la Kibra kwenye mji mkuu wa Nairobi.

Raila Odinga ambaye ni mpinzani mkubwa wa William Ruto kutoka muungano wa Kenya Kwanza na Naibu Rais wa Kenya, alifika kituoni hapo akiwa amesindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo lenye idadi kubwa ya watu, zamani likijulikana kama Kibera.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa uchaguzi huo umekuwa mzuri, na ni matumaini yake utamalizika vizuri.