Obama, Lady Gaga na BTS kuhutubia mahafali ya 2020 YouTube

0
579

Mtandao wa YouTube kipitia ‘YouTube Originals’ umeandaa mahafali kwa wahitimu wa mwaka 2020 duniani yatakayofanyika Juni 6, ikiwa ni sehemu ya kuwaunganisha wahitimu, kutokana na uwepo kwa ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19).

Mahafali hayo yatakayokwenda kwa jina la “Dear Class of 2020” yatarushwa mubashara katika ukurasa wa ‘YouTube Originals’.

“Mahafali ni utamaduni ambao wanafunzi na familia wanasubiria kwa hamu, kwa hali ya sasa ya ulimwengu, YouTube inasaidia kwa kutuletea mahafali kwa uhalisia zaidi,” mkuu wa maudhui ya YouTube duniani ameiambia Variety.

Watakaohutubia katika mahafali hayo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, pamoja na mkewe Michelle Obama, wanamuziki wa Korea Kusini-kikundi cha BTS, Lady Gaga, Katibu Mstaafu wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleezza Rice na mwanadada mdogo zaidi kupokea tuzo ya kimataifa ya heshima ya “Nobel Prize Laurete,” Malala Yousafzai.

Mgeni rasmi wa shughuli hiyo bado amefanywa siri hadi hapo mahafali yatakapoanza.

Wahitimu wanaweza kusaini majina yao katika ubao wa salamu wa “Dear Class of 2020 Shout Out Board” kupitia kiunganishi hiki https://yt.be/dearclassof2020

Mahafali hayo yatarushwa YouTube Originals kupitia kiunganishi (https://www.youtube.com/channel/UCqVDpXKLmKeBU_yyt_QkItQ na ukurasa wa YouTube wa Learn@Home ( https://learnathome.withyoutube.com/) na ratiba nzima ya siku hiyo itawekwa katika ukurasa huu Mei 17.

Mbali na BTS wasanii wengine kama vile; AsapSCIENCE, Kelly Rowland, Alicia Keys, Mr. Kate, Zendaya Chloe x Halle, The Try Guys, Kerry Washington, Dude Perfect, Zane Hijazi na Jackie Aina watatumbuiza baada ya mahafali hayo (after-party).

Mahafali ya namna hii yamefanyika pia nchini Japan ambapo Chou Kikuu cha Biashara (Business BreakThrough) kilifanya mahafali yake kwa kutumia roboti zilizovalishwa joho na kuunganishwa na programu tumishi ya ZOOM.