Ntaganda kwenda gerezani miaka 30

0
786

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yenye Makao Makuu yake mjini The Hague nchini Uholanzi, imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani, aliyekuwa kiongozi wa Waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC),- Bosco Ntaganda.

Ntaganda amehukumiwa adhabu hiyo baada ya ICC kumtia hatiani kwa makosa 18 aliyokuwa ameshtakiwa kuyatenda.

Miongoni mwa makosa hayo ni mauaji pamoja na vitendo vya udhalishaji alivyokua akivifanya dhidi ya Wanawake.

Ntaganda katika kipindi chote cha miaka mitatu ya kusikilizwa kwa kesi yake amekua akisisitiza kuwa hana hatia.

Mbabe huyo wa Kivita mwenye umri wa miaka 45, alishtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa kusimamia mauaji ya Raia pamoja na askari wake kwenye eneo la Ituri lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika kipindi cha mwaka 2002 na 2003.