Nimepona UVIKO

0
265

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametangaza kuwa kwa sasa amepona kabisa na hana tena maambukizi ya UVIKO – 19.

June 07, 2023 Rais Museveni alitangaza hadharani kuwa na maambukizi ya UVIKO-19, lakini kwa sasa amesema baada ya siku 11 za kupambana na ugonjwa huo yuko mzima wa afya.

Katika siku zote hizo za ugonjwa wake kulikuwa na taarifa mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika mitandao ya kijamii kuhusu hali yake.

Rais Museveni amewataka Wananchi wa Uganda kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo.