Niger kuomboleza kwa siku tatu

0
136

Serikali ya Niger imetangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa, kufuatia kuuawa kwa takribani watu mia moja nchini humo.

Mauaji hayo yanadhaniwa kufanywa na Wanamgambo katika vijiji viwili vya
Tchombangou na Zaroumdareye, vilivyopo katika eneo la mpaka wa nchi ya Niger na Mali.

Pamoja na kutangaza siku hizo tatu za maombolezo, Rais Mahamadou Issoufou wa Niger, pia ameitisha kikao.cha Baraza la Usalama la Taifa kwa lengo la kujadili hali ya usalama nchini humo.

Tayari Serikali ya Niger imepeleka vikosi zaidi katika jimbo la Tillabéri, ambalo limekuwa likikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara yanayodaiwa kufanywa na vikundi mbalimbali vya Wanamgambo.