Ndege ya kijeshi yapotea

0
503

Ndege ya kijeshi ya Chile iliyokuwa na watu 38 imeripotiwa  kupotea baada ya kuruka kutoka kituo cha kijeshi cha Antarctica nchini humo.

Ndege hiyo inaelezwa kuondoka saa kumi na moja jioni ya jana na ilipofika saa kumi na mbili mawasiliano yalipotea.

Habari zinaeleza kuwa hwenda ndege hiyo imeanguka huku  jitihada za kuitafuta zikiendelea .

Miongoni mwa waliotoweka na ndege hiyo ni wafanyakazi 17 na abiria 21 ambao walikuwa wakisafiri.

Jenerali wa jeshi nchini hymo Eduardo Mosqueira amesema  ndege hiyo haikuonyesha dalili zozote za tatizo kabla ya kuondoka.

Rais Sebastian Pinera wa Chile kupitia ukurasa wake wa  Twitter amesema amesikitishwa na taarifa za kutoweka kwa ndege hiyo na kwamba anafanya uchunguzi kwa mamlaka ya hali ya hewa mjini santiago kujua wapi ndege hiyo ipo.