Nchi za Ulaya kuinusuru Iran

0
910

Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya zimetafuta njia mpya za kufanya malipo kwa baadhi ya kampuni zinazofanya biashara na Iran, ili kuinusuru nchi hiyo kiuchumi baada ya Marekani kuiwekea vikwazo vipya.


Mpango huo mpya wa nchi hizo za Umoja wa Ulaya unapingana na mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani, aliyetangaza kuiwekea Iran vikwazo vipya kwa madai kuwa nchi hiyo haiaminiki kutokana na mpango wake wa nyuklia.


Trump alitupilia mbali mkataba wa awali uliokuwa umefikiwa kati ya nchi hiyo na Iran, pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ambayo awali iliridhika na hatua ambayo nchi hiyo ilikuwa imefikia kufanya marekebisho katika mpango wake wa nyuklia.


Uamuzi wa Marekani wa kuiwekea Iran vikwazo vipya haukukubaliwa na Umoja wa nchi za Ulaya, licha ya Marekani kutishia kuichukulia hatua nchi yoyote itakayokiuka vikwazo hivyo vipya.


Nchi za Umoja wa Ulaya hivi sasa zimeamua kupitishia malipo ya kibiashara yanayofanywa na kampuni za nchi hizo pamoja na Iran kwenye bara hilo wakitumia sarafu za Ulaya, badala ya kutumia Dola za Kimarekani ili kuepuka vikwazo vya nchi hiyo.