Nchi ndogo zaidi duniani, ina Raia 30

0
574

Molossia ni nchi iliyojitambulisha yenyewe kuwa nchi na hivyo kuwa nchi ndogo zaidi duniani yenye raia 30 na wanayama aina ya mbwa wanne pekee.

Nchi hiyo imeanzishwa mwaka 1977, inapatikana mashariki mwa jimbo la Nevada nchini Marekani.

Molossia ni nchi ndogo zaidi duniani licha ya kuwa na eneo la ardhi lenye hekari 6.3 huku ikiwa haina hospitali wala shule ndani yake.

Nchi hiyo inakaliwa na idadi kubwa ya wanaume ikilinganishwa na wanawake, kutokana na hali ya hewa ya nchi hiyo kuonekana kuwafaa zaidi wanaume kwani hali ya hewa ni ya jangwa.

Kutokana na sababu za eneo la nchi hii kuwepo katikati ya jangwa, hakuna kilimo wala mazao yanayopatikana nchini humo huku pia kukiwa hakuna barabara za lami wala viwanja vya ndege.

Nchi hiyo ya Molossia ilianzishwa na Kevin Baugh mwenye umri wa miaka 60 na ambaye kwa sasa ndiye anayehudumu kama Rais na kiongozi wa Taifa hilo linalojiita Jamhuri ya Molossia.

Licha ya nchi hiyo kujitangaza kama nchi, haijakubaliwa kutambulika hivyo na serikali yoyote ama Umoja wa Mataifa.

Taifa hilo limefanikiwa kuwa na utambulisho wake wa kipekee ukiutofautisha na nchi zingine, sarafu yake na mfumo wa sheria na taratibu za nchi hiyo.

Sarafu rasmi ya Molossia inafahamika kama Valora na katika Taifa hilo hakuna utaratibu wa kulipa kodi.

Kama zilivyo nchi zingine, Molossia ina ofisi za kiserikali pamoja na wimbo wa Taifa.

Ingawa kingereza ni lugha rasmi ya nchi hiyo, Kiesperanto kinatambulika rasmi kama lugha ya pili.