NCHI 10 ZENYE FURAHA ZAIDI DUNIANI MWAKA 2022

0
1686

Ripoti ya Dunia ya Furaha ya mwaka 2022 imetoka na kuonesha kuwa nchi ya Finland ndio nchi ambayo wananchi wake wanafuraha zaidi ulimwenguni kwa sasa.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa nchi za Scandinavia zimeshika nafasi za juu za wananchi wake kuwa na furaha kwa mwaka 2022 huku Uswis, Uholanzi, Lexembourg na Iceland nazo zikiorodheshwa katika Top Ten
Kwa mujibu wa chapisho lililotolewa na Taasisi ya kukusanya Data ya Gallup World Poll imesema ripoti ya Dunia ya Furaha inaangazia furaha duniani kote lakini pia mataifa yenye furaha zaidi, yale yaliyo chini kabisa ya kiwango cha furaha.

Nchi zilizo katika orodha ya kumi bora kati ya nchi zenye furaha zaidi Duniani ni kama ifuatavyo:-

  1. Finland
  2. Denmark
  3. Iceland
  4. Switzerland
  5. Netherlands
  6. Luxembourg
  7. Sweden
  8. Norway
  9. Israel
  10. New Zealand