Rais Hage Geingob wa Namibia ametangaza hali ya tahadhari nchini humo baada ya ukame kuyakumba maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Akitangaza hali hiyo, Rais Geingob ameziagiza taasisi zote nchini humo kushirikiana kuhakikisha raia wa nchi hiyo wanasaidiwa kwa hali na mali katika kukabiliana na hali hiyo ya ukame.
Kwa mujibu wa Rais Geingob, msimu wa mvua nchini Namibia umemalizika bila nchi hiyo kupata mvua, hivyo hali imeendelea kuwa mbaya zaidi.