Mzee Mkapa amfagilia Mzee Moi

0
323

Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa amesema kuwa eneo la Afrika Mashariki litaendelea kumkumbuka Rais wa Pili wa Kenya, Mzee Daniel Arap Moi kwa jitihada zake za kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mzee Mkapa ameyasema hayo jijini Nairobi nchini Kenya katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC).

Rais huyo mstaafu yupo nchini Kenya kuongoza ujumbe wa Tanzania katika mazishi ya Mzee Moi yanayofanyika leo katika mji wa Kabarak.

Amesema ndani ya kipindi cha miaka saba alichofanya kazi karibu na Mzee Moi, walishirikiana kuimarisha mshikamano baina ya wananchi wa Tanzania na Kenya.

Kwa mujibu wa Rais Mkapa, Moi alisimamia umoja, amani, upendo, na mshikamano, vitu ambavyo ni muhimu katika kuwaletea wananchi maendeleo.