Mwili wa Mwanamfalme Philip wapumzishwa leo

0
169

Mwili wa Mume wa Malkia wa Uingereza (Malkia Elizabeth II), Mwanamfalme Philip aliyefariki Aprili 9 mwaka huu akiwana miaka 99, unazikwa kwenye nyumba ya milele leo Aprili 17, katika mji wa Windsor baada ya kukamilika kwa taratibu zote za mazishi ya kifalme.

Mwanamfalme Philip na Malkia Elizabeth II wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka 73 hadi umauti ulipomfika Philip.

April 10, mizinga 41 tofauti na ilivyozoeleka, ilipigwa Uingereza kwa heshima ya Mwanamfalme Philip ‘Duke of Edinburgh’.

Kufuatia kuwepo kwa janga la COVID-19, na ushauri wa wataalamu wa afya, wananchi wameombwa kuepuka mikusanyiko na kufika kuweka maua kwenye makasri ya familia ya malkia, badala yake wameombwa kutoa misaada kwa wenye uhitaji.

Aidha, kitabu cha maombolezo ya mume wa Malkia Elizabeth II kimewekwa mtandaoni kwa wale wote ambao wangependa kutoa salamu za rambirambi.

Uingereza ipo kwenye kipindi cha maombolezo ya kitaifa kwa siku tisa, huku wanafamilia wakiwa katika kipindi cha wiki mbili tangu kifo chake.