Mamia ya Raia wa Zimbabwe wanatajiwa kujitokeza kwa wingi katika barabara mbalimbali za mji mkuu wan chi hiyo Harare, kuupokea mwili wa Rais wa zamani wan chi hiyo Robert Mugabe unaowasili nchini humo ukitokea Singapore.
Habari kutoka nchini Zimbabwe zinaeleza kuwa, tayari mwili wa Kiongozi huyo wa zamani wan chi hiyo umekwishasafirishwa kutoka nchini Singapore na utapokelewa katika uwanja wa Ngege ulopo mjini Hahrare mchana huu.
Mugabe alifariki Dunia nchini Singapore wiki iliyopita, alipokwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu tangu mwezi Aprili mwaka huu.
Magari yaliyopambwa na na yale ya kuongeza misafarara pamoja na farasi, wameoneana katika uwanja huo wa ndege uliopo mjini Harare, tayari kwa mapokezi ya mwili wa Robert Mugabe.
Mara baada Mwili wa Mzee Mugabe kuwasili nchini Zimbabwe, raia wa nchini watapewa muda wa siku Mbili kwa ajili ya kuuaga kabla ya kufanyika kwa mazishi.
Habari Zaidi kutoka nchini Zimbabwe zinaeleza kuwa, mpaka sasa kumekua na mfulizo wa vikao kati ya viongozi wa serikali na familia ya Mzee Mugabe kwa lengo la kujadili mahali atakapozikwa shujaa huyo.
Kumekua na taarifa zinazoeleza kuwa, familia ya Mzee Mugabe ingependelea azikwa kijijni kwake alikozaliwa na si mahali palipoandaliwa na serkali kwa ajili ya mazishi ya viongozi ama watu mashuhuri nchini humo na kwamba haitaki mazishi hayo yahudhuriwe na watu watu waliojusika kumuondoa madarakani mwezi Novemba mwaka 2018.
