Mwili wa Malkia Elizabeth II utazikwa na mwili wa mumewe ambao awali ulikuwa umehifadhiwa sehemu maalum kwa mwaka mmoja kwa lengo la kusubiri upumzishwe na wa mkewe Malkia Elizabeth II pindi atakapofariki.
Malkia Elizabeth II amefariki akiwa na umri wa miaka 96 mwili wake unatarajiwa kupumzishwa siku ya Jumatatu 19, 2022 huko Windsor Castle.
Hata hivyo kwa taratibu za utawala huo wa kifalme mwili wa aliyekuwa mume wa malkia Elizabeth II ,Prince Philip ambaye alifariki April 09, 2021 akiwa na umri wa miaka 99 ulikuwa umehifadhiwa kwenye sehemu maalum katika nyumba ya ibada ya St George’s Chapel kwa masharti kwamba mahali pakupumzisha rasmi mwili wake patakuwa ni kando ya mwili wa mke wake atakapofariki hivyo basi utazikwa kando ya mwili wa Malkia Elizabeth II siku ya Jumatatu 19, 2022.