Mwafrika wa kwanza kuathirika na virusi vya Corona apona

0
428

Mwanafunzi mwenye uraia wa Cameroon nchini China aliyekuwa chini ya uangalizi maalum, amepona kabisa homa ya virusi vya Corona baada ya kupatiwa matibabu.

Kem Senou Pavel Daryl (21), aligundulika kuwa na virusi vya corona na baada ya kukaa kwenye karantini huku akipewa viuavijasumu (antibiotics) pamoja na dawa wanazopewa waathirika wa UKIMWI aliweza kupona ndani ya wiki mbili.

Daryl ni Mwafrika wakwanza aliyethibitishwa kuumwa homa ya Corona na wakwanza kupona.

Wakati akiumwa alikataa kurudi Afrika akisema kuwa hakutaka kuleta maradhi hayo Afrika kwani tayari anapewa matibabu bure nchini China.