Upande wa upinzani katika jimbo la Hong Kong nchini China unashinikiza kupitishwa kwa muswada wa kupinga kura ya kutokuwa na imani na Meya wa jimbo la Hong Kong, baada ya meya huyo kukiri kuwa yeye ndiye aliyehamasisha muswada wa watu wa kisiwa hicho kwenda kushitakiwa bara.
Meya huyo, ikiwa imepita siku moja alikiri, kuhamasisha mabadiliko ya haraka, kuhusiana na muswada huo uliopingwa vikali na wakazi wa kisiwa cha Hong Kong, wakisema kuwa unawanyima haki yao ya msingi na maana ya uhuru wa kisiwa chao.
Muswada huo ulisababisha maandamano makubwa kwenye kisiwa hicho, ambapo wakati mwingine polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kupambana na waandamanaji waliovuka vizuizi vya polisi.