Rais wa zamani wa Zimbabwe, -Robert Mugabe, anatarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo nchini humo.
Msemaji wa Serikali ya Zimbabwe, -George Charamba amesema kuwa, mwili wa Mugabe utasafirishwa kutoka nchini Singapore kwenda nchini humo siku ya Jumatano.
Mugabe alifariki dunia siku ya Ijumaa nchini Singapore, alikokua akipatiwa matibabu.
Amekua Rais wa Zimbabwe kwa muda wa miaka 37 hadi mwaka 2017 alipoachia wadhifa huo.