Mubarak afariki dunia akiwa na Miaka 91

0
325

Rais wa zamani wa Misri, – Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo  mwaka 2011, amefariki dunia mjini Cairo akiwa na umri wa miaka 91.

Mubarak aliiongoza Misri kwa vipindi vitatu kabla ya kutokea kwa maandamano ya muda mrefu yaliyosababisha jeshi kuingilia kati na hivyo kumuondoa madarakani.

Kifo cha Mubarak kimetangazwa na vyombo mbalimbali vya habari vya Serikali ya Misri, huku habari zaidi zikieleza kuwa amefariki dunia katika hospitali moja ya kijeshi.

Mwezi Januari mwaka huu Mubarak alifanyiwa upasuaji, na baada ya upasuaji huo ikatangazwa kuwa hali yake inaendelea vizuri.