Mtu wa tatu kuugua Ebola nchini Uganda afariki dunia

0
356

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kufariki dunia kwa mgonjwa waTatuwa Ebola katika mji wa Kasese, ambaye ni msichana mwenye umri wa miaka Tisa.

Msichana huyo aliingia nchini Uganda akitokea katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo – DRC.

Sampuli ya damu ya msichana huyo ilifanyiwa uchunguzi na kuthibitishwa kuwa anaugonjwa wa Ebola na ndipo baadaye alihamishiwa kwenye kituo cha kuwapatia matibabu wagonjwawa Ebola.

Wakati hayo yakitokea nchini Uganda, wizara ya Afya katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesemakuwa, mpaka sasa watu Elfu Mbili wamethibitika kufariki dunia baada ya kuugua ugonjwa huo.