Mtoto wa Kagame ajiunga kumlinda baba yake

0
287

Mtoto wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, Luteni Ian Kagame amejiunga na kikosi cha ulinzi wa Rais kilicho chini ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF).

Kikosi cha ulinzi cha Rais wa Rwanda kinawajibika kumlinda Rais pamoja na familia yake.

Ian alionekana hadharani kwa mara ya kwanza akitimiza majukumu yake mpya wakati wa maombi ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Jumapili iliyopita.

Maombi hayo ambayo hufanyika kila mwaka, yalihudhiriwa pia na Rais Kagame na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali wa serikali ya Rwanda pamoja na viongozi wa dini.

Ian ni mhitimu wa chuo cha kijeshi cha Sandhurst cha nchini Uingereza.