Mtendaji mkuu wa Hong Kong amewaomba radhi

0
295

Mtendaji mkuu wa Hong Kong Carrie Lam amewaomba radhi raia wote wa Hong Kong kwa namna alivyosimamia muswada tata wa kuruhusu kusafirishwa kwa wahalifu wa Hong Kong kwenda kushitakiwa katika mahakama za nchini China.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, kiongozi huyo amesema anawajibika moja kwa moja na namna Muswada huo ulivyopokelewa na kuzua taharuki na maandamano makubwa ya kupinga muswada huo ambao umesitishwa.

Hata hivyo, kiongozi huyo hakuweka bayana iwapo ataendeleza mjadala wa muswada huo au kujiuzulu kutokana na baadhi ya waandamanaji kumtaka ajiuzulu madarakani kufutia maandamano ya kutaka kufutwa kabisa kwa muswada huo.

Hong Kong iliyokuwa chini ya Utawala wa Uingereza, ilikabidhiwa rasmi na kuwa sehemu ya  China mwaka 1997, katika mfumo wa nchi moja yenye mifumo miwili ya utawala.