Mtangazaji maarufu Larry King afariki dunia

0
271

Mtangazaji mkongwe na maarufu wa nchini Marekani, – Larry King amefariki dunia mjini Los Angeles akiwa na umri wa miaka 87.

Habari kutoka nchini humo zinaeleza kuwa Larry King amefariki dunia katika hospitali ya Cedars-Sinai.

Katika uhai wake, Larry King amepata umaarufu mkubwa kutokana na vipindi vyake vya mahojiano mbashara hasa akiwa kituo cha Televisheni cha CNN, alivyofanya na Watu mashuhuri wakiwemo Wanasiasa, Wasanii na Wanamichezo.

Katika siku za hivi karibuni kulikuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Larry King yupo hospitalini akipatiwa matibabu zaidi baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Pia katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo.