Baadhi ya Wakazi wa jimbo la Colorado nchini Marekani wamelazimika kuyahama makazi yao, kufuatia moto pori unaowaka na kuteketeza nyumba na mali mbalimbali yakiwemo magari.
Watu Saba wamejeruhiwa katika tukio hilo, ambapo moto huo unaelezwa kusambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali.
Zaidi ya Wakazi elfu ishirini katika mji wa Louisville na wengine elfu 13 kwenye mji wa Superior wamehamishiwa katika maeneo ya usalama kufuatia moto huo.
Vikozi vya zimamoto vinaendelea kukabiliana na moto huo, huku uongozi wa jimbo la Colorado ukitangaza hali ya tahadhari