Moto waua 38 gereza la Gitega

0
201

Watu 38 wamefariki dunia na wengine 69 wamejeruhiwa baada ya moto kuteketeza sehemu ya gereza la Gitega nchini Burundi.

Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza amesema moto huo umeharibu sehemu kubwa ya gereza hilo ambalo ni kubwa kuliko yote katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura, gereza ambalo pia lina idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu.

Miongoni mwa vitu vilivyoteketea katika moto huo ni magodoro na vitu vingine vilivyokuwa ndani ya mabweni ya gereza hilo kubwa la Gitega.

Mwezi Agosti mwaka huu, moto ulizuka katika gereza hilo ambapo maafisa wa gereza walisema ulisababishwa na hitilafu ya umeme.