Moto wasababisha vifo vya watu 70 Bangladesh

0
864

Watu sabini wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya moto mkubwa kuzuka katika ghorofa moja la makazi ya watu kwenye mji wa Dhaka nchini Bangladesh.

Jengo hilo la ghorofa licha ya kuwa makazi ya watu, pia lilikuwa na eneo linalotumika kama ghala.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa,  mlipuko mkubwa ulitokea ndani ya ghala lililoko katika jengo hilo la ghorofa.

Mlipuko huo ulianzia kwenye mtungi wa kemikali ambazo zimekuwa zikitumika kutengenzea marashi na baada ya kulipuka moto huo uliruka na kwenda kulipua mtungu wa gesi uliokuwa katika mgahawa jirani na ghala hilo.

Mara baada ya mitungi hiyo miwili kulipuka, mmoja ukiwa wa kemikali na mwingine wa gesi, moto ulianza kusambaa katika maeneo ya jirani na kuanza kuhatarisha usalama.

Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo hilo.

Matukio ya majengo marefu kuwaka moto yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini Bangladesh,  hasa katika viwanda vya nguo.