Moto wa msituni wawatesa wakazi wa Perth

0
167

Uongozi wa mji wa Perth nchini Australia, umewataka wakazi wa mji huo kubaki ndani ya nyumba zao, wakati askari wa vikosi vya zimamoto na uokoaji wakiendelea kupambana kuzima moto wa msituni karibu na makazi yao.

Moto huo umeendelea kuwaka kwa kasi na kuanza kusogelea makazi ya watu, na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Uongozi wa mji wa Perth umesema kuwa, itakuwa salama endapo watu watabaki ndani kwani moshi mkubwa umekuwa ukifuka na kuhatarisha usalama.

Watu 60 wamelazimika kuhamishwa kutoka katika makazi yao, wengi wao wakiwa ni wale wanaoishi katika kijiji kimoja cha Wastaafu.