Moshi watanda katika miji ya Sydney na Adelaide

0
750

Moshi uliosababishwa na moto wa msituni nchini Australia, umetanda katika miji mikubwa ya Sydney na Adelaide.

Habari zinasema kuwa, Maafisa Afya nchini Australia wametoa tahadhari kuhusu hali ya hewa, huku baadhi ya Wakazi wa mji wa Sydney wakifunika nyuso zao kujikinga na hewa chafu.

Waziri Mkuu wa Australia, – Scott Morrison ametetea Sera ya mabadiliko ya Tabia Nchi ya Serikali yake na kusema kuwa haijachangia katika athari za moto nchini humo.

Katika kipindi cha mwezi mmoja, watu Sita wamefariki Dunia nchini humo kutokana na moto wa msituni katika maeneo ya New South Wales na Queensland, yaliyopo Mashariki mwa nchi hiyo.